Utafiti wa WHO waonesha watu nane kati ya kumi wanaishi maeneo yenye hewa chafu
Shirika la Afya duniani - WHO limesema uchafuzi wa hewa umekuwa chanzo cha vifo vya mamilioni ya watu ambapo utafiti unaonesha kuwa watu WANANE kati ya KUMI duniani kote wanaishi katika maeneo yenye hewa iliyochafuliwa

Utafiti huo umefanyika katika maeneo tofauti ELFU TATU duniani kote. Kwa mwaka 2012 pekee inakadiriwa kuwa vifo vya watu milioni 6 na Laki TANO sawa na asilimia 11.6 vimehusishwa na uchafuzi wa hewa.

Kwa mujibu wa WHO magonjwa hayo yanayosababishwa na uvutaji wa hewa chafu hayaambukizi mengi yakiwa ni yale ya moyo na saratani ya mapafu.

Awali taarifa iliyotolewa na umoja wa mataifa kuhusiana na uchafuzi wa hewa inasema asilimia 80 watu wanaoishi miji duniani kote wanavuta hewa iliyochafuliwa.

 

 September 27, 2016

JUDICA LOSAI

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI