OBAMA ahutubia kwa mara ya mwisho mkutano wa UN
Rais BARACK OBAMA wa MAREKANI amehutubia kwa mara ya mwisho Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Rais BARACK OBAMA wa MAREKANI amehutubia kwa mara ya mwisho Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kabla ya kumaliza muda wake wa urais mwezi Januari mwakani.

Katika hotuba yake, Rais OBAMA ameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa mataifa mbalimbali.

Aidha amesema uchumi wa dunia umeimarika kutoka kwenye mdororo wa kifedha wa mwaka 2008 na pia makubaliano yamefikiwa kuhusu mpango wa nyuklia wa IRAN.

Hata hivyo amebainisha kuwa dunia inaendelea kukumbana na matatizo kama vile ugaidi na wakimbizi wanaokimbia mapigano pamoja na mataifa yenye nguvu yanayopingana na vikwazo vilivyowekwa dhidi yao na sheria za kimataifa.

Rais OBAMA pia amesema anahofu ya kuongezeka kwa misimamo mikali ya utaifa, misingi ya imani kali za kidini na mifumo ya serikali inayofuata misingi hiyo.

 

 

September 21, 2016

MARTHA NGWIRA

==  == = 

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI