Watoto walio katika mazingira hatarishi kusaidiwa
Serikali imeandaa mpango mkakati wa kuwabaini na kuwatambua watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kufanya kazi hatarishi mitaani ili kuwaondoa katika hali hiyo kwa kuwaunganisha na familia zao.
Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Serikali imeandaa mpango mkakati wa kuwabaini na kuwatambua watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kufanya kazi hatarishi mitaani ili kuwaondoa katika hali hiyo kwa kuwaunganisha na familia zao.

​Katika kikao na waandishi wa habari mjini DODOMA, Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesema mkakati huo utawaunganisha watoto hao na taasisi mbalimbali zitakazo wasimamia ili kuwatoa katika mazingira hatarishi.

Maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii hufanyika tarehe 21 mwezi Machi kila mwaka duniani kote na kauli mbiu mwaka huu inasema USTAWI WA JAMII, KUKUZA NA KUIMARISHA JAMII NA MAZINGIRA.

VICTORIA PATRICK

MACHI 20, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI