Marufuku kutumia simu wakati wa kutoa huduma
Wauguzi na madaktari mkoani SIMIYU wametakiwa kuacha tabia ya kupiga na kupokea simu wakati wa kutoa huduma kwani tabia hiyo inapunguza umakini katika utoaji wa huduma licha ya kwamba ni kinyume na maadili ya kazi.
Katibu tawala wa mkoa wa SIMIYU, JUMANNE SAGINI

Wauguzi na madaktari mkoani SIMIYU wametakiwa kuacha tabia ya kupiga na kupokea simu wakati wa kutoa huduma kwani tabia hiyo inapunguza umakini katika utoaji wa huduma licha ya kwamba ni kinyume na maadili ya kazi.

Agizo hilo limetolewa na katibu tawala wa mkoa wa SIMIYU JUMANNE SAGINI wakati wa  uzinduzi wa mradi wa Mkunga okoa maisha uliofanyika  mjini BARIADI.

Mradi huo unalengo la kubadili tabia ya jamii ili kuwajengea tabia ya akina mama kujifungua katika vituo vya afya ili kupunguza vifo vya wajawazito na watoto.

Mradi wa Mkunga Okoa Maisha unatekelezwa mkoani Simiyu kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka march 2017 hadi Machi 2020.

PASCHAL MICHAEL

MACHI 20, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI