Halmashauri zatakiwa kulipa gharama za nyumba za NHC
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi ANGELINA MABULA ameagiza halmashauri ambazo zimeshindwa kutimiza makubaliano ya mkataba ya kulipa gharama za nyumba walizojengewa na shirika la nyumba- NHC.
Naibu waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi Angelina Mabula akitoa maelekezo ya uboreshaji wa miradi inayotekelezwa na shirika la nyumba nchini, alipotembelea mradi wa nyumba wa Safari City Arusha.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi ANGELINA MABULA ameagiza halmashauri ambazo zimeshindwa kutimiza makubaliano ya mkataba ya kulipa gharama za nyumba walizojengewa na shirika la nyumba- NHC.

Naibu Waziri MABULA ametoa agizo hilo jijini ARUSHA baada ya kukagua ujenzi wa nyumba za gharama nafuu za mradi wa NHC wa SAFARI CITY wenye viwanja zaidi ya mia sita.

Kwa upande wake meneja washirika la nyumba mkoa wa ARUSHA, JAMES KISARIKA amesema katika mradi wa SAFARI CITY,  tayari wameshauza viwanja mia MOJA HAMSINI,  kati ya MIASITA.

Safari CITY ni mradi  unaosimamiwa na shirika la Nyumba Nchini wenye ekari zaidi ya MIATANO na unatarajiwa kuwa mji wa kisasa wenye ofisi, nyumba za ngarama nafuu, za kati, za juu,  shule,  na huduma za jamii ikiwemo bustani zamapumziko.

JUSTIN MSECHU

MACHI 20, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI