Fedha za zamani biashara jijini DSM
Katika hali unayoweza kuona siyo ya kawaida, biashara ya fedha za zamani inafanyika jijini DSM na wateja wakubwa ni watu wanaotaka kuziweka fedha hizo kuwa kumbukumbu.
Noti ya zamani ya shilingi mia moja za Kitanzania.

Katika hali unayoweza kuona siyo ya kawaida, biashara ya fedha za zamani inafanyika jijini DSM na wateja wakubwa  ni watu wanaotaka kuziweka fedha hizo kuwa kumbukumbu.

Mwandishi wa TBC amefanya mahojiano na mfanyabiashara  MARTIN SHABAN katika eneo la Mnazi mmoja ambaye amesema fedha hizo ambazo ni sarafu za senti moja hadi shilingi moja pamoja na noti zilizotumika nchini kuanzia enzi za ukoloni hadi miaka ya tisini pia hutumika katika masuala ya kimila.

Amesema fedha hizo huzinunua kutoka kwa watu mbalimbali na kisha huziuza kwa faida.

VUMILIA MWASHA

MACHI 20, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI