Timu ya Korea Kusini kucheza na Simba na Yanga
Ubalozi wa Korea Kusini hapa nchini umesema umepanga kuileta moja ya timu ya ligi kuu ya nchini Korea Kusini kuja kucheza michezo ya kirafiki ya kimataifa na timu za Simba na Yanga mwishoni mwa mwezi june au july mwaka huu.
Balozi wa Korea Kusini, Song Geum Young

Ubalozi wa Korea Kusini hapa nchini umesema umepanga kuileta moja ya timu ya ligi kuu ya nchini Korea Kusini kuja  kucheza michezo ya kirafiki ya kimataifa na timu za Simba na Yanga mwishoni mwa mwezi june au july mwaka huu.

Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Song Geum Young  amesema wanapanga kuileta timu hiyo hapa nchini ili kuboresha urafiki uliopo baina ya Tanzania na Korea Kusini  huku mkurugenzi mkuu wa shirika la utangazaji nchini Ayub Rioba akipongeza kwa hatua hiyo ya Korea Kusini kuleta timu hapa nchini.

Balozi huyo pia amezungumzia mchezo wa TAIKONDO ambapo amesema hivi sasa wapo walimu kutoka Korea Kusini wanaotoa mafunzo kwa wachezaji wa mchezo huo hapa nchini.

NORA ULEDI

MACHI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI