BMT yawataka wadau wa mchezo wa mashua kugombea nafasi za uongozi
Baraza la michezo la TAIFA, BMT limewataka wadau wa mchezo wa mashua kujitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi wa nafasi mbalimbali katika chama hicho kwani mpaka sasa bado zoezi la uchukuaji fomu linasuasua.

Msemaji wa BMT, NAJAH amesema ni watu sita waliochukua fomu bila kujua wanawania nafasi gani katika chama hicho kwani uchaguzi umepangwa kufanyika MARCH 28 mwaka huu.

Nafasi zinazowaniwa ni mwenyekiti, katibu, ,mweka hazina pamoja na wajumbe wanne katika chama hicho.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI