Pangani wabadili ofisi kuwa Zahanati
Wakazi wa kata ta PANGANI katika halmashauri ya mji wa KIBAHA mkoani PWANI wameamua kubadilisha matumizi ya jengo la ofisi ya serikali ya mtaa wa KIDIMU kuwa Zahanati .

Wakazi wa kata ta PANGANI katika halmashauri ya mji wa KIBAHA mkoani PWANI wameamua kubadilisha matumizi ya jengo la ofisi ya serikali ya mtaa wa KIDIMU kuwa zahanati.

 

Wakazi hao wamefikia uamuzi huo wakati wa mkutano mkuu kutokana na adha waliyokuwa wakiipata ya kutembea zaidi ya kilometa 12 kwenda kufuata huduma za matibabu katika kituo cha afya mkoani.

 

Mkutano huo umehudhuriwa na wakazi wa kata hiyo ya PANGANI ambapo wamechangia shilingi milioni tatu za kukarabati jengo hilo.

 

Kwa upande wake mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa KIBAHA Dokta TULITWENI MWINUKA amewashauri wakazi hao kupanua majengo hayo ili yaweze kukithi vigenzo vilivyowekwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii.

 

 

JOSEPH CHEWALE

MACHI10, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI