Sudan Kusini yatakiwa kuchunguzwa
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limetoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu mashambulizi ya silaha za kemikali yaliyofanywa na Serikali ya SUDAN dhidi ya raia katika eneo la DARFUR Magharibi mwa nchi hiyo.
SUDAN

Katika ripoti yake mpya Amnesty International imetaka kufanyike uchunguzi kamili kuhusu mashambulizi ya silaha za kemikali yaliyofanyika katika miezi ya Januari hadi Disemba mwaka jana katika Jimbo la DARFUR. 

Taarifa iliyotolewa na maafisa wa Umoja wa Mataifa imeashiria mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa na Jeshi la Serikali ya SUDAN katika eneo la JABAL MURRAH katika Jimbo DARFUR na kusema kuwa kushindwa kwa wajumbe wa Jumuiya ya Kuzuia Silaha za Kemikali -OPCW kufanya uchunguzi kuhusu suala hilo kunatia aibu na fedheha kubwa.

Ripoti hiyo ilikadiria kuwa watu kati ya 200 na 250 waliuawa katika mashambulizi hayo ya silaha za kemikali na kwamba wengi wao walikuwa watoto wadogo.

Mwaka 2009 na 2010 Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ilitoa hati ya kukamatwa kwa Rais OMAR AL-BASHIR kwa tuhuma za makosa ya kufanya kivita, makosa dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari katika eneo la DARFUR.     

GHANIA JUMBE

MACHI 08, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI