Shirikisho la muziki Tanzania wampongeza rais MAGUFULI kwa utendaji wake
Shirikisho la wa Muziki Tanzania limempongeza Rais JOHN MAGUFULI kwa kuchaguliwa kuliongoza taifa na kuunga mkono
ADDO NOVEMBA

Shirikisho la wa Muziki Tanzania limempongeza Rais JOHN MAGUFULI kwa kuchaguliwa kuliongoza taifa na kuunga mkono kasi aliyoanza nayo katika utendaji kazi wake.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini DSM  Rais wa Shirikisho hilo ADDO NOVEMBA amesema kuwa ziara hizo za rais siyo tu ameonesha kutosha Kwenye Kiti bali amekuwa mtetezi wa wanyonge.

 

ADDO amesema “Ziara za Ghafla za Rais MAGUFULI siyo za kubezwa Ni za kupongezwa sana. Japo kuna wenye roho mbaya na wasioitakia mema nchi yetu wanabeza maana wao walizoea kubweteka na kufurahia wanyonge wakiteseka.”

 

Shirikisho la Muziki Tanzania tumeona matunda ya Rais Magufuli juzi amekwenda Muhimbili na Jana tangazo limetoka kuwa mashine za MRI zimeanza Kufanya Kazi hili jambo si la kubezwa hata kidogo bila jitihada binafsi za Ndugu Magufuli leo watanzania wangeendelea kufa na kukata tamaa kwa kukosa matibabu. 

 

Ndugu wanahabari haikuwa rahisi kwa wakati Kama huu ambao Ni wa Kupanga serikali mpya bado Rais ametoa Muda wa kwenda kuhakikisha wanyonge wanapata matibabu na huduma tuna pongezi sana Ndugu Magufuli.

 

Wamemuomba rais MAGUFULI aendelee na wembe huo huo wa  Ziara hizo za kushtukiza maeneo mengi ambayo wameeleza  yana uozo na  azibe mianya ya wakwepa kodi hasa Kwenye madini ambako amedai kuna Mikatana mibovu, wizi na usafirishaji haramu wa madini, Ni Jambo la aibu Tanzanite kwa wingi ipo

“Kwa kuziba mianya hiyo na kuleta maendeleo ya wote hakika hatutahitaji misaada ya wazungu. Tupo tayari kufunga Mkanda kwa miaka hii mitano ili kuacha hazina kwa Taifa letu lenye kila aina ya utajiri.” Aliongeza ADDO

 

Pia shirikisho hilo limemtakia  afya njema na kuahidi kushirikiana naye Kwenye haki za wanamuziki Kama alivyoahidi alipokutana na wanamuziki na wasanii jijini DSM Mlimani City vile vilena kumuombea kwa Mungu apate Baraza la Mawaziri dogo lenye ufanisi na kupunguza mzigo kwa serikali Kama dhamira yake alivyoionesha Kwenye kuondoa safari za Nje.

 

Kwa upande mwingine shirikisho hilo limewapongeza wasanii wote walioshiriki Kwenye kampeni za vyama mbali mbali na kuwaeleza Sasa kampeni zimeisha Ni Muda wa Kufanya Kazi, wawe pamoja na rais MAGUFULI kushirikiana katika kujiletea maendeleo yao wenyewe.

 

Katika kuonesha kumuunga mkono Rais MAGUFULI shirikisho hilo linaandaa Mkutano Mkubwa wa Amani na Maandamano ya kuunga Mkono Hatua za rais Magufuli kwakuwa  wana imani na wanaamini Mungu atamuwezesha kuyatimiza yote na kukata Kiu ya watanzania.

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI