Watu wawili watekwa nyara nchini Kenya
Watu wenye silaha wamewateka nyara walimu wawili raia wa Kenya karibu na kambi ya wakimbizi ya Dadaab, iliyo kaskazini mashariki mwa Kenya na kuwasafirisha kwenda Somalia.
Kambi ya wakimbizi ya DAADAB ambayo ipo karibu na eneo tukio la utekaji lilipotokea

Watu wenye silaha wamewateka nyara walimu wawili raia wa Kenya karibu na kambi ya wakimbizi ya Dadaab, iliyo kaskazini mashariki mwa Kenya na kuwasafirisha  kwenda Somalia.

Habari  zimesema watu hao walivamia nyumbani kwa walimu hao waliokuwa wanasoma kwenye shule moja ya binafsi katika kambi ya wakimbizi ya Hagardheere ambayo ni moja ya kambi za Dadaab.

Habari zimesema kutokana na hali ya wasiwasi ilivyokuwa katika kambi ya Dadaab, serikali ya Kenya ilitangaza kuifunga kambi hiyo kwa sababu za kiusalama.

Hata hivyo mahakama kuu ya Kenya hivi majuzi iliamuru kuwa hatua hiyo ni kinyume na katiba na ukiukaji wa haki kwa kuwa karibu watu laki tatu walikuwa wakiishi kwenye kambi hiyo.

MARTHA NGWIRA

MACHI 3, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI