Kamishna MIHAYO atoa tathmini ya mapambano ya Dawa za Kulevya
Kamishina wa operesheni ya Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya MIHAYO MSIKHERA amesema wamefanikiwa kukamata kete 328 za dawa za kulevya aina ya Heroin na kuteketeza ekari 93 za mashamba ya bangi
Kete za Madawa ya Kulevya

Kamishina wa operesheni ya Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya MIHAYO MSIKHERA amesema wamefanikiwa kukamata kete 328 za dawa za kulevya aina ya  Heroin na kuteketeza ekari 93 za mashamba ya bangi katika mikoa 15 waliyofanya operesheni ya kuwakamata watuhumiwa wa dawa za kukevya.


Akitoa tathmini ya operesheni iliyofanyika kwa siku nne nchini, MSIKHERA amesema kuwa pia wamewakamata watumishi wawili wa serikali kwa kuingiza nchini kemikali  inayotumika kutengenezea dawa za kulevya.


Amesema wamekamata idadi kubwa ya kete za Heroine katika mkoa wa SONGWE na LINDI  huku ekari nyingi za mashamba ya bangi zikiteketezwa katika mikoa ya kipolisi ya TARIME na RORYA mkoani MARA.
 

Aidha amewataka wananchi kutojihusisha na biashara na matumizi ya dawa za Kulevya kwa kuwafichua watu wanaojihusisha na biashara hiyo.

 

 

MBOZI KATALA

FEBRUARI 17, 2017 

 

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI