Waziri Mkuu azindua Baraza la Taifa la Kudhibiti Dawa za Kulevya
Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amewataka viongozi wa serikali na wale wa vyombo vya ulinzi na usalama kuzingatia sheria, weledi na kushirikisha wananchi kuanzia ngazi za chini ili kufanikisha mapambano dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya.
Kamishna Mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia Madawa ya Kulevya Nchini Rogers William Sianga akijitambulisha mbele ya Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya wakati Waziri Mkuu alipokuwa akizindua Baraza Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.

Waziri Mkuu KASSIM MAJALIWA amewataka viongozi wa serikali na wale wa vyombo vya ulinzi na usalama kuzingatia  sheria, weledi na kushirikisha wananchi kuanzia ngazi za chini ili kufanikisha mapambano dhidi ya biashara na matumizi  ya dawa za kulevya.

 

Waziri Mkuu MAJALIWA amesema hayo jijini DSM  wakati akizindua Baraza la Taifa la Kudhibiti Dawa za Kulevya linalowahusisha mawaziri na makatibu wakuu kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, wakuu wa mikoa yenye hadhi ya Majiji na iliyopembezoni mwa nchi pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama.

 

Takwimu za mapambano ya dawa za kulevya zinaonesha katika kipindi cha kuanzia January 2015 hadi Desemba 2016 vyombo vya dola vimefanikiwa kukamata kilo 77 za dawa za kulevya aina ya  Heroin zikihusisha kesi 703 na kilo 32 za COCAINE zikihusisha kesi 259.

 

Katika uzinduzi wa baraza hilo Waziri Mkuu MAJALIWA amewataka wajumbe wa baraza hilo kushirikisha wananchi na kueleza mikakati iliyopo ya kudhibiti uingizaji na usafirishaji wa dawa hizo katika maeneo ya mipakani.

 

Aidha waziri Mkuu MAJALIWA amesema serikali imekamilisha mpango wa kudhibiti biashara ya pombe haramu.

 

Baraza la Taifa la Kudhibiti Dawa za Kulevya lilianzishwa chini ya kifungu cha 5 cha sheria ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya na 5 cha mwaka 2015.

 

 

MBOZI KATALA

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI