Benki ya Uarabuni kuwekeza kwenye sekta ya kilimo
Benki ya Uarabuni, UBL imesema iko tayari kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Kilimo ambayo itawezesha Tanzania kupata fursa ya kuweza kuuza mazao yake katika nchi za ughaibuni.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. PHILIP MPANGO

Benki ya Uarabuni, UBL imesema iko tayari kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Kilimo ambayo itawezesha Tanzania kupata fursa ya kuweza kuuza mazao yake katika nchi za ughaibuni.

Akizungumza na waziri wa Fedha na Mipango Dr. PHILIP MPANGO jijini DSM, Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo FAISAL JAMALL amesema dhamira ya UBL ni kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji, uboreshaji wa mifugo na uvuvi nchini Tanzania.

Naye DR. Mpango amesema  uchumi wa Tanzania umeimarika na Jumuiya ya Mabenki imeanza kuwa na imani na Tanzania na kitendo cha Benki ya UBL kuonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya kilimo kutaharakisha maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini.

VUMILIA MWASHA

FEBRUARI 17, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI