Wakurugenzi watakiwa kuwalipa wakandarasi kwa wakati
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya uwajibikaji wa umma nchini WIPA LUDOVIC UTTOH amesema watendaji wakuu wa taasisi za umma wanatakiwa kubadilika ili kuendana na masharti ya mikataba na wakandarasi wanapotekeleza miradi ya maendeleo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya uwajibikaji wa umma nchini-WIPA, LUDOVIC UTTOH

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya uwajibikaji wa umma nchini WIPA LUDOVIC UTTOH amesema watendaji wakuu wa taasisi za umma wanatakiwa kubadilika ili kuendana na masharti ya mikataba na wakandarasi wanapotekeleza miradi ya maendeleo.

 

akizungumza jijini DSM wakati taasisi yake ikitoa mafunzo kwa wakurugenzi wa taasisi za umma UTTOH amesema kuwajibika kwao ni pamoja na kuwalipa wakandarasi kwa wakati ili kuepuka kulundikana kwa faini zinazotozwa baada ya kukiuka mikataba

 

naye mkurugenzi wa utetezi na maboresho wa taasisi ya LHRC ANNA HEGA amesema wakurugenzi wengi wanashindwa kuwajibika kuwalipa wakandarasi kwa wakati kutokana na kuweka bajeti ndogo kulingana na hali halisi ya thamani ya miradi.

 

 

STANLEY GANZEL

FEBRUARI 16, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI