Wananchi wa LUSHOTO waishukuru serikali kwa kuwajengea daraja
Wananchi wa vijiji vya MIEGEO na ZETA wilaya ya LUSHOTO mkoani TANGA wameishukuru serikali kwa kuwaondolea adha ya usafiri kwa kuwajengea daraja katika mto ZETA .

Wananchi wa vijiji vya MIEGEO na ZETA wilaya ya LUSHOTO mkoani TANGA wameishukuru serikali kwa kuwaondolea adha ya usafiri kwa kuwajengea daraja katika mto ZETA .

 

Wakazi hao wamesema kwa muda mrefu walikuwa wakisafiri umbali mrefu kufuata huduma ya usafiri kwenye vijiji jirani kwa kuwa magari yalikuwa hayawezi kufika kijijini kwao kutokana na  kutokuwepo na daraja katika mto huo.

 

Ujenzi wa daraja hilo ambalo awali ulikadiriwa kugharimu shilingi milioni mia moja lakini kwa sasa limejengwa kwa shilingi milioni nane tu utasaidia  kuinua uchumi wa wakazi wa vijiji hivyo vya MIEGEO na ZETA.

 

Akizindua daraja hilo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya LUSHOTO, LUCAS SHEMNDOLWA amewataka wakazi hao kuhifadhi mazingira ili daraja hilo liweze kudumu kwa muda mrefu.

 

 

JOACHIM KAPEMBE

FEBRUARI 15, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI