Madaktari saba wahukumiwa kwenda jela kwa kuidharau Mahakama
Mahakama Kuu ya KENYA imewahukumu kifungo cha mwezi mmoja jela maafisa saba wa chama cha madaktari wa nchi hiyo kwa kuidharau amri ya mahakama

Mahakama Kuu ya KENYA imewahukumu kifungo cha mwezi mmoja jela maafisa saba wa chama cha madaktari wa nchi hiyo kwa kuidharau amri ya mahakama hiyo ya kuwataka kuumaliza mgomo wa madaktari nchini humo.

Mgomo huo wa madaktari umeathiri huduma katika hospitali za umma kwa wiki kumi sasa.

Jaji HELLEN WASILWAT wa mahakama hiyo  amesema viongozi hao hawakutoa sababu za kuridhisha kuonyesha ni kwa nini walishindwa kumaliza mgomo huo.

Mgomo huo wa madaktari umeanza mwishoni mwa mwaka jana  na kusababisha hospitali za umwa kufungwa na wagonjwa kushindwa kupata huduma  ipasavyo.

Madaktari wamekuwa wakiitaka serikali kuheshimu makubaliano ya mwaka 2013 ya kuwaongezea mishahara.

 

 

MARTHA NGWIRA

Februari 13, 2017

 == = = =

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI