KOREA KASKAZINI yashutumiwa kwa jaribio la kombora
Nchi ya JAPAN na KOREA KUSINI zimeshutumu vikali jaribio lingine la kombora la masafa ya kati lililofanywa na nchi jirani ya KOREA KASKAZINI

Nchi ya JAPAN na KOREA KUSINI zimeshutumu vikali jaribio lingine la kombora la masafa ya kati lililofanywa na nchi jirani ya KOREA KASKAZINI na kusema kuwa kitendo hicho hakiwezi kuvumilika kwani ni uchokozi.

Nchi hizo zinasema KOREA KASKAZINI imekuwa ikivunja wazi mikataba ya Umoja wa Mataifa kwa kufanya majaribo yake hayo ya makombora, zimejipanga kuiadhibu nchi hiyo.

Wachunguzi wa masuala ya kimataifa wanasubiri kwa hamu kauli ya rais wa MAREKANI, DONALD TRUMP, baada ya KOREA KASKAZINI kufanya jaribio lake hilo la kombora katika bahari inayozitenganisha nchi hizo na JAPAN.

Wakati wa kampeni zake za uchaguzi TRUMP alitangaza kuwa hatavumilia uchokozi wowote utakaofanywa na nchi ya KOREA YA KASKAZINI, hata hivyo baadhi ya wachunguzi wa siasa za MAREKANI wanasema TRUMP analazimia kuchukua hatua za taratibu kutokana na changamoto za wahamiaji zinazolikabili taifa lake.

 

 

HERIETH SHIJA

Februari 13, 2017

==

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI