Maandamano ya kupinga ukatili dhidi ya watu weusi nchini UFARANSA yazaa ghasia
Maandamano ya kupinga vitendo vya utakatili vinavyofanywa na askari wa UFARANSA dhidi ya watu weusi nchini UFARANSA,

Maandamano ya kupinga vitendo vya utakatili vinavyofanywa na askari wa UFARANSA dhidi ya watu weusi nchini UFARANSA, yalianza kwa amani, lakini baadaye yakageuka kuwa ghasia katika mji wa BOBIINII.

Waandamanaji walikuwa wakiandamana kupinga taarifa za kijana mmoja mwenye asili ya AFRIKA kudhalilishwa kijinsia akiwa mikononi mwa polisi na hatimaye kulazimika kualazwa hospitalini na kufanywa upasuaji.

Waandamanaji wanasema wanashindwa kuamini maneno ya polisi kuwa matuhumiwa alidhalilishwa kijinsia kwa bahati mbaya. Wanasema wameandamana kupinga vitendo vya uonevu kwa weusi, ambavyo pia vinaweza kufanyika kwa mtu yeyote.

Maandamano kama hayo wiki iliyopita yalisababisha ghasia na baadhi ya waandamanji kuchoma moto magari. Askari polisi wanne wamesimamishwa kazi kutokana na tukio hilo, wakipisha uchunguzi, huku askari mmoja akifunguliwa mashtaka ya kuhusika na vitendo vya ubakaji.

 

 

NYAMBONA MASAMBA

FEBRUARI 12,2017     

===

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI