Wadau wa afya watakiwa kuhamasisha utoaji wa huduma za afya vijijini
Watoa huduma ya afya nchini wameshauriwa kuhamasisha taasisi, kampuni na watu binafsi kuchangia usambazaji wa utoaji wa huduma ya afya vijijini

Watoa huduma ya afya nchini wameshauriwa kuhamasisha taasisi, kampuni na watu binafsi kuchangia usambazaji wa utoaji wa huduma ya afya vijijini ili kuweza kuwafikiwa wananchi wanaoishi pembezoni.

Ushauri huo umetolewa mkoani Mwanza  na Mhadhiri wa Chuo kikuu kishiriki cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili MUHAS, Dkt PETER DATTANI  ambapo amesema wapo wataalamu wengi wa kitanzania wenye uwezo wa kutoa huduma za afya vijijni endapo kampuni na taasisi zitahamasishwa kugharamia zoezi hilo.

Dkt  DATTANI amesema hivi sasa  Timu ya madaktari bingwa sita ,waganga na wauguzi kutoka nchi ya  KOREA KUSINI wapo mkoani MWANZA kwa ajili ya kutoa huduma za afya bure kwa wananchi na kuomba wadau kusaidia kupeleka huduma hiyo vijijini.

Timu nyingine ya madaktari kutoka MAREKANI inatarajiwa kuwasili nchini February 20 mwaka huu  kutoa huduma ya matibabu kwa wakazi wa visiwani na Mwambao wa ziwa VICTORIA kupitia shirika la CHRISTIAN WORLD LIFE MISSION FRONTIER.   

 

 

REGINALD NDESIKA

FEBRUARI 13,2017

=====

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI