Makao Makuu ya nchi ya EQUATORIAL GUINEA yahamishwa
Serikali ya EQUATORIAL GUINEA imehamisha makao yake makuu kutoka katika Mji Pwani wa MALABO kwenda katika Mji ulioko kwenye Ukanda wa Msitu wa Mvua wa DJIBLOHO

Serikali ya EQUATORIAL GUINEA imehamisha makao yake makuu kutoka katika Mji Pwani wa MALABO kwenda katika Mji ulioko kwenye Ukanda wa Msitu wa Mvua wa DJIBLOHO.

 

Rais TEODORO OBIANG NGUEMA wa EQUATORIAL GUINEA amesema amechagua eneo jipya la DJIBLOHO kama moja ya miji anayotaka kuiendeleza kwa kutumia utajiri wa mafuta wa nchi hiyo.

 

Mji huo uko karibu na mbuga nyingi za taifa za nchi hiyo.

 

Waziri Mkuu FRANCISCO PASCUAL OBAMA ASUE amewaonya wabunge wasitumie muda wa kukaa huko kama mapumziko.

 

 

GHANIA JUMBE

Februari 9, 2017

= = = =

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI