MYANMAR kuchunguzwa kuhusu raia wake wanaodaiwa kuuwawa
Serikali ya MYANMAR, imesema kuwa itafanya uchunguzi kuhusiana na taarifa kuwa raia wa nchi hiyo ambao ni waislamu kutoka katika kabila la ROHINGYA

Serikali ya MYANMAR, imesema kuwa itafanya uchunguzi kuhusiana na taarifa kuwa raia wa nchi hiyo ambao ni waislamu kutoka katika kabila la ROHINGYA waliuawa kwa makusudi na askari wa nchi hiyo, katika ukaguzi maalum uliofanywa na jeshi.

Tangazo la serikali ya nchi hiyo limekuja huku meli ya misaada, ikiwasili nchini humo kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali ya kibinadamu.

Misaada hiyo ya kibinadamu iliyowasili kwa meli ni kwa ajili ya watu wa jamii ya ROHINGYA, wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhaba wa chakula. Msaada huo pia utatolewa kwa kabila lingine dogo.

Hivi karibuni vyombo vya habari vilitoa picha za askari wa MYANMAR, wakiwatesa na kuwaua watu wa jamii ya ROHINGYA.

 

 

NYAMBONA MASAMBA

Februari 9, 2017

==

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI