Rais mpya wa SOMALIA akabiliwa na kibarua kigumu
Habari kutoka nchini SOMALIA zinasema, rais mpya wa nchi hiyo, aliyechaguliwa jana na bunge, HASSAN SHEIKH MAHMOUD anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuliongoza taifa

Habari kutoka nchini SOMALIA zinasema, rais mpya wa nchi hiyo, aliyechaguliwa jana na bunge, HASSAN SHEIKH MAHMOUD anakabiliwa na changamoto kubwa ya kuliongoza taifa ambalo limeshuhudia kwa miongo kadhaa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Bunge la SOMALIA ndio limelazimika kumchagua rais mpya kutokana na hali ya usalama nchini huko.

Jana ulinzi uliimarishwa nchini SOMALIA na hakukuwa na ndege iliyoruhusiwa kuruka katika anga la nchi hiyo.

Hata hivyo kulikuwa na taarifa ya vifo vya watu wanne katika shambulio la kigaidi lililofanywa na wapiganaji wa kikundi cha AL SHABAAB, huko PUNTLAND.

 

 

NYAMBONA MASAMBA

Februari 9, 2017

==

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI