LUPEMBE FC yaanza maandalizi ya Mwenge
Timu ya LUPEMBE FC ya wanawake Manispaa ya MPANDA imeanza maandalizi ya mashindano ya uwashaji MWENGE Kitaifa mkoani KATAVI

Timu  ya  LUPEMBE FC ya wanawake  Manispaa  ya  MPANDA imeanza maandalizi  ya mashindano  ya uwashaji  MWENGE Kitaifa  mkoani  KATAVI  ambapo  timu  mbalimbali  zimejiandikisha  kushiriki  mashindano  hayo  mwishoni  mwa mwezi  wa  tatu mwaka  huu.

Mwandishi  wa TBC   ametembelea mazoezi  ya  timu  hiyo  na kufanya mahojiano  na  baadhi  ya  wachezaji  juu maandalizi ya  mashindano  hayo.

Akizungumzia  maandalizi  ya  timu  hiyo  kepteni  wa  timu  hiyo  ya wanawake   LAURENCIA SANGA amesema wameanza  maandalizi  hayo   pia  kwa  ajili  ya  kucheza  katika  mashindano  mbalimbali  baada  ya kuwashwa  kwa  MWENGE wa Uhuru April mbili.

SANGA pamoja  na mchezaji  Hubwa Diwani wamesema wanajivunia uongozi uliopo  na  kuahidi ushindi.

 

 

Adolph Mbata

Februari 3, 2017

= = = ==

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI