WESTHAM yamshukia PAYET kwa utovu wa nidhamu
Klabu ya WESTHAM UNITED wamemshushia tuhuma nzito nyota wao DIMITRI PAYET kwa kutoonyesha heshima kwao na kukosa nia thabiti ya kuitumikia klabu yao

Klabu ya WESTHAM UNITED wamemshushia tuhuma nzito nyota wao DIMITRI PAYET  kwa kutoonyesha heshima kwao na kukosa nia thabiti ya kuitumikia klabu yao, kufuatia nyota huyo kujiunga tena na klabu yake ya zamani ya OLIMPIKI MARSEILLE kwa ada ya uhamisho ya paundi millioni 25.

Wagonga nyundo hao wa LONDON wamesisitiza kuwa hawakuwa na mpango kabisa wa kumuuza PAYET ambapo mwenyekiti mwenza wa WESTHAM UNITED, DAVID SULLIVAN AMESISITIZA KUWA walitaka nyota huyo abakie katika klabu yao.

SULLIVAN anasema PAYET ameuzwa kutokana na kocha wa WESTHAM  SLAVEN BILICH kukubali hilo ili kuweka umoja katika kikosi hicho.

PAYET amesaini mkataba wa miaka MINEE na nusu kuitumikia klabu yake ya zamani ya olympic marseile.

 

 

ENOCK BWIGANE

30 Januari 2017

====

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI