Wanawake wanaojitoa mhanga NIGERIA waja na mbinu ya kuwabeba watoto
Serikali ya NIGERIA imeonya kuwa wanawake wanaojitoa mhanga nchini humo wanawabeba watoto wachanga mgongoni ili wasiweze kutiliwa mashaka wakati wanapofanya mashambulio.

Serikali ya NIGERIA imeonya kuwa wanawake wanaojitoa mhanga nchini humo wanawabeba watoto wachanga mgongoni ili wasiweze kutiliwa mashaka wakati wanapofanya mashambulio.

Onyo hilo limetolewa kufuatia wanawake wawili waliokuwa wamebeba watoto mgongoni kufanya mashambulio ya kujitoa mhanga katika mji wa MADAGALI siku 10 zilizopita.

Wanawake hao Januari 13 mwaka huu walipita kwenye kizuizi lakini hawakutiliwa mashaka kwa kuwa walikuwa wamebeba watoto na hivyo kusababisha vifo vya watu wanne, wao wenyewe pamoja na watoto waliokuwa wamewabeba.

MARTHA NGWIRA

JANUARI 24, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI