Manchester United yaifunga Hull City
Manchester United imejiwekea mazingira mazuri ya kutinga katika fainali ya michuano ya kombe la ligi nchini England baada ya kuifunga Hull City bao 2-0.
Mchezaji wa Manchester United Juan Mata akiifungia tmu yake bao la kwanza katika mchezo wa Kombe la Ligi nchini England dhidi ya Hull City. Manchester United ilishinda kwa mabao 2-0 na kujiweka katika nafasi nzuri ya kucheza fainali ya kombe hilo.

Manchester United imejiwekea mazingira mazuri ya kutinga katika fainali ya michuano ya kombe la ligi nchini England baada ya kuifunga Hull City bao 2-0.Mchezo huo ni wa nusu fainali ya kwanza baina ya timu hizo huku mechi ya marudiano ikipangwa kufanyika baada ya wiki mbili ambapo mshindi wa jumla atatinga katika fainali dhidi ya Liverpool au Southampton.Juan Mata alitangulia kuipatia United bao la kwanza kipindi cha pili baada ya kumaliza kipindi cha kwanza matokeo yakiwa ni sare ya bila kufungana huku Maruane Fellaini akifunga bao la pili lililohakikishia ushindi kwa Man United katika dimba la Old Trafford.

 

 

JANE JOHN

JANUARI 11, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI