Vyama vya michezo vyatakiwa kuwasilisha mipango kazi
Baraza la Michezo la Taifa – BMT limeviagiza vyama vya michezo nchini kupeleka mipango kazi yao ya kushiriki mashindano yajayo ya kimataifa kabla ya Januari 24 kwenye baraza hilo ili iweze kufanyiwa kazi kwa pamoja.
Katibu Mkuu wa BMT, Mohamed Kiganja

Baraza la Michezo la Taifa – BMT limeviagiza vyama vya michezo nchini kupeleka mipango kazi yao ya kushiriki mashindano yajayo ya kimataifa kabla ya Januari 24 kwenye baraza hilo ili iweze kufanyiwa kazi kwa pamoja.

Akizungumza na TBC jijini Dar Es Salaam, Katibu Mkuu wa BMT, Mohamed Kiganja amesema mipango kazi hiyo ya vyama vyote vya michezo nchini ikipatikana itasaidia kuiwekea mikakati ya utekelezaji kwa pamoja kama taifa.

Tanzania itashiriki mashindano ya kimataifa ya All Africa Games, Jumuiya ya Madola na Olympiki itakayofanyika Japan mwaka 2020, hivyo vyama vya michezo vimeamua kujipanga mapema kutafuta mbinu za ushindi kabla ya kushiriki michuano hiyo.

JANE JOHN

JANUARI 11, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI