Diamond akabidhiwa bendera ya taifa
Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye amemkabidhi bendera ya taifa msanii wa muziki wa kizazi kipya Nasib Abdul (Diamond) anayetarajia kwenda nchini Gabon kutumbuiza katika ufunguzi kombe la mataifa ya Afrika-AFCON 2017.
Nasib Abdul (Diamond)

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amemkabidhi bendera ya taifa msanii wa muziki wa kizazi kipya Nasib Abdul maarufu kama Diamond ambaye anatarajia kwenda nchini Gabon kutumbuiza katika ufunguzi wa michuano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika -AFCON 2017.

 

Akimkabidhi bendera hiyo Waziri Nape amesema msanii Diamond kutoa burudani katika ufunguzi wa michuano ya AFCON kutasaidia kuwatangaza wasanii wa Tanzania na Tanzania kwa ujumla.

 

Katika hatua nyingine Waziri Nape amesema atahakikisha sheria ya sanaa inafanyiwa marekebisho ili wasanii wafaidike na kazi wanazozifanya.

 

Michuano ya kombe la mataifa ya Afrika - AFCON inatarajiwa kuanza kutimua vumbi January 14 mwaka huu nchini Gabon.

 

 

JANE JOHN

JANUARI 11, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI