NEEC waagizwa kutekeleza sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi
Serikali imeiagiza bodi mpya ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi-NEEC- kuhakikisha utekelezaji wa sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi unafanyika kwa vitendo na inaleta manufaa kwa wananchi.
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, kazi, vijana, ajira na walemavu JENISTA MHAGAMA akisisitiza jambo katika uzinduzi wa bodi mpya ya Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi, NEEC

Serikali imeiagiza bodi mpya ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi-NEEC- kuhakikisha utekelezaji wa sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi unafanyika kwa vitendo na inaleta manufaa kwa wananchi.

Akizindua bodi hiyo jijini DAR ES SALAAM, Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, kazi, vijana, ajira na walemavu JENISTA MHAGAMA amesema bodi inapaswa kuhakikisha sera hiyo inatekelezwa katika taasisi zote za umma na binafsi.

Naye mwenyekiti wa bodi hiyo  DKT. JOHN JINGU amesema  bodi yake imedhamiria kuchochea utekelezaji wa sera hiyo katika ngazi zote za uchumi ili Tanzania iweze kufikia nchi ya uchumi wa kati ifikapo 2025.

VUMILIA MWASHA

JANUARI 10, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI