Ukubwa wa mtaji wapungua soko la hisa la DSE
Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizohorodheshwa katika soko la hisa la DAR ES SALAAM, DSE umeshuka kutokana na kupungua kwa bei ya hisa zikiwemo hisa za kampuni ya TBL na benki ya CRDB.
Afisa mwandamizi wa DSE, PATRIC MUSUSA

Ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizohorodheshwa katika soko la hisa la DAR ES SALAAM, DSE umeshuka kutokana na kupungua kwa bei ya hisa zikiwemo hisa za kampuni ya TBL na benki ya CRDB.

 Akitoa tathmini ya soko lilofanyika wiki iliyopita, Afisa mwandamizi wa DSE, PATRIC MUSUSA amesema mtaji umeshuka kutoka shilingi tirioni 19 wiki iliyotangulia hadi kufikia shilingi tirioni 18.6.

Amesema mauzo ya hisa  yameongezeka kwa asilimia 59  kutoka shilingi bilioni 8.3 na kufikia shilingi bilioni 13.2 huku idadi ya hisa zilizouzwa  na kununuliwa zimeongezeka kutoka milioni 1.3 wiki iliyotangulia na kufikia shilingi milioni 2.8.

VUMILIA MWASHA

JANUARI 10,2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI