Mapigano yasambaa IVORY COAST
Mapigano kati ya maafisa wa jeshi nchini IVORY COAST yamesambaa katika miji SITA ya nchi hiyo.
Majeshi ya IVORY COAST mjini BOUAKE

Mapigano kati ya maafisa wa jeshi nchini IVORY COAST yamesambaa katika miji SITA ya nchi hiyo.

 

Milio ya risasi imesikika katika mji mkuu wa kibiashara wa ABIJAN na mji wa PILI kwa ukubwa nchini humo wa BOUAKE unashikiliwa na jeshi.

 

Jeshi hilo limeziba njia zote za kuingilia kwenye mji huo wenye watu zaidi ya nusu milioni.

 

Majeshi hayo yanadai kuongezewa mishahara na kuboreshwa kwa marupurupu pamoja na maeneo ya kazi ambapo waziri wa ulinzi wa IVORY COAST amesema serikali iko tayari kusikiliza madai ya wanajeshi hao walioasi.

 

 

JUDICA LOSAI

JANUARI 07, 2017

MOST POPULAR
+
+
HABARI ZINAZO HUSIANA
ZILIZOSOMWA ZAIDI