Responsive image
Responsive image
Posted : September 13, 2015 (3 years ago) By TBC
Responsive image
Mkuu wa Majeshi wa BURUNDI anusurika kufa
Responsive image

Mkuu wa majeshi wa BURUNDI, Jenerali PRIME NIYONGABO, amenusurika kuuwawa baada ya msafara wake kushambuliwa katika mji mkuu, BUJUMBURA.   

Naibu mkuu wa polisi, Jenerali GODEFROID BIZIMANA amesema watu SABA wameuawa kwenye mashambulizi hayo wakiwemo washambuliaji WAWILI ambapo mmoja wao amekamatwa.

Afisa mwingine wa polisi amesema walinzi WANNE wa Jenerali huyo pamoja na afisa mmoja wa polisi mwanamke wameuwawa.

Mashuhuda wanasema washambuliaji walikuwa wamevalia sare za kijeshi na walikuwa kwenye gari la kijeshi.

Polisi wamesema inawatafuta washambuliaji wengine, ambao wanatuhumiwa kuwa wa kikosi cha makamando

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment