Responsive image
Responsive image
Posted : September 11, 2015 (3 years ago) By TBC
Responsive image
TWIGA STARS yafungwa 3-0
Responsive image

Nchini CONGO BRAZZAVILLE kwenye michuano ya ALL AFRICA GAMES timu ya taifa ya TANZANIA ya wanawake TWIGA STARS imekubali kichapo cha pili kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa na NIGERIA bao TATU kwa bila.

Huu ni mchezo wa pili kwa timu hiyo kupoteza baada ya kufungwa na IVORY COAST bao moja kwa bila katika mchezo wa kwanza.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo la A IVORY COAST imechomoza na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya CONGO.

Kwa matokeo hayo timu za NIGERIA na IVORY COAST zina pointi SITA kila moja huku TANZANIA na CONGO zikiwa hazina pointi hata moja baada ya kufungwa michezo miwili ya kwanza.

 

Mchezo mwingine kwa TWIGA STARS utakua siku ya jumamosi pale watakapokutana na CONGO huku NIGERIA ikikutana na IVORY COAST.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment