Responsive image
Responsive image
Posted : May 17, 2018 (6 days ago) By TBC
Responsive image
Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia sare za jeshi zinazoshonwa na kiwanda cha ushonaji nguo baada ya kuzindua rasmi kituo cha uwekezaji cha JWTZ kupitia SUMA-JKT kilichopo Mgulani jijini Dar es salaam.
Responsive image

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amezindua kituo cha uwekezaji cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kilichopo katika kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani (831KJ) Jijini Dar es Salaam.

Kituo hicho kina viwanda vya kushona nguo, kutengeneza maji, kukereza vyuma na pia kina chuo cha ufundi stadi (VETA), shule ya sekondari Jitegemee na kumbi mbili za mikutano (Muhuga Hall na Isamuhyo Hall). Uwekezaji wote umegharimu Shilingi Bilioni 5.7.

Rais Magufuli pia ametembelea kiwanda cha ushonaji wa nguo kilichogharimu Shilingi Milioni 810 na ambacho kina uwezo wa kushona jozi 500 za sare za askari kwa siku na kuzalisha ajira za watu 350, na pia ametembelea kiwanda cha kutengeneza maji ambacho kimegharimu Shilingi Bilioni 1.6 na kina uwezo wa kuzalisha chupa 3,600 za maji kwa saa.

Akizungumza katika mkutano uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali Magufuli ameipongeza JWTZ kupitia Shirika lake la SUMAJKT kwa kuitikia vizuri wito wake wa kujenga viwanda na ameahidi kuwa serikali itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi hilo katika jukumu la kujenga uchumi wa nchi kupitia viwanda na shughuli nyingine za uzalishaji mali.

“Naomba nimpongeze Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuyo kwa jitihada alizozifanya kujenga miradi hii akiwa Mkuu wa JKT, nampongeza Mkuu wa JKT wa sasa na SUMAJKT kwa kazi nzuri mnayoifanya, kwa kweli leo nimefurahi sana kuona jeshi letu linajenga viwanda, huu ni mwelekeo mzuri, askari wetu sasa watashonewa nguo kutoka hapa hapa nchini kwetu” amesema. 

Magufuli pia ametoa wito kwa majeshi yote nchini kununua sare kutoka viwanda vya majeshi na kwa upande wa maji ametoa wito kwa Watanzania kunywa maji ya Uhuru Peak yanayotengenezwa na SUMAJKT zikiwemo ofisi za umma, na amesema kuwa uwekezaji huo utasaidia JWTZ kupata mapato kwa ajili ya kujiendesha na kupunguza ukubwa wa fedha za bajeti kutoka serikalini.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment