Responsive image
Responsive image
Posted : May 15, 2018 (a week ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt. John Magufuli akwahoji kuhusu mafuta ya kula maofisa aliowakuta bandarini Dar es Salaam katika ziara yake ya kushtukiza. Picha na MIchuzi blog
Responsive image

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumanne amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoza kodi zinazostahili kwa mafuta ya kula baada ya kubainika kuwa baadhi ya wafanyabiashara wamefanya udanganyifu.

Rais pia ameruhusu mafuta ya kula yaliyohifadhiwa katika matanki ya Kurasini kusambazwa ili kuepusha upungufu wa mafuta ya kula unaoweza kujitokeza.

Agizo la Magufuli kwa TRA liliegemea kwenye ripoti ya timu ya uchunguzi wa mafuta ya kula iliyoongozwa na Prof. Joseph Buchweishaija, ambayo baada ya kuyachunguza matanki 43 yenye tani 105,630 za mafuta ya kula ilibaini kuwa kati ya matanki hayo, saba yana  mafuta yaliyoboreshwa (refined oil), 14 mafuta yaliyoboreshwa kiasi (semi refined oil), manne ni mafuta ya kutengenezea sabuni na 18 ni mafuta ghafi (crude oil).

Matokeo hayo yamepishana na taarifa zilizowasilishwa TRA na kampuni za uagizaji mafuta za Vegetable Oil Terminal (VOT), Tanzania Liquid Storage (TLS) na East Coast Oils and Fats Limited (EC) ambazo zilionesha kuwa sehemu kubwa ya mafuta hayo ni ghafi. Mafuta ghafi hutozwa kodi ya asilimia 10 tu wakati yale yaliyoboreshwa hutozwa asilimia 25.

 Rais Magufuli ameagiza mafuta yote yanayostahili kutozwa kodi ya asilimia 10 yatozwe hivyo, yanayostahili kutozwa kodi asilimia 25 yatozwe kwa kiwango hicho na wafanyabiashara wote waliofanya udanganyifu kwa kuonesha kuwa mafuta yao ni ghafi wakati sio ghafi wapigwe faini kwa mujibu wa sheria na mafuta yaanze kusambazwa haraka iwezekanavyo.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment