Responsive image
Responsive image
Posted : May 15, 2018 (a week ago) By TBC
Responsive image
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba (aliyeketi kulia) akitia saini makubaliano ya kutangaza kombe la dunia kwa kushirikiana na Kwese Free Sports kupitia luninga ya TV1. Aliyeketi kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Kwese Free Sports, Joseph Sayi.
Responsive image

Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) limezindua kutangaza matangazo ya kombe la Dunia kwa kushirikiana na  kampuni ya Kwese Free Sports kupitia kituo chao cha luninga cha TV1.

Uzinduzi huo umefanyika katika ofisi za TBC Mikocheni jijini Dar es Salaam leo Jumanne ambapo Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba na Mkurugenzi Mkuu wa Kwese Free Sports Josepi Sayi walisaini makubaliano hayo.

Mkurugenzi wa Masoko wa TBC, Daphrosa Kimbori amesema TBC ni chombo cha umma na ndio maana kimeingia makubaliano hayo huku Meneja masoko wa TV1 Giriani Rugumamu akiwataka Watanzania kutumia fursa hiyo kujitangaza. 

Kombe la Dunia litaonyeshwa kupitia vituo vya luninga vya TBC1 na TV1 na pia litatangazwa kupitia Radio ya Taifa ya TBC Taifa.

Matangazo hayo yatakuwa ni bure na Kwa mara ya kwanza matangazo hayo  ya michezo yote ya kombe la Dunia yatatangazwa kwa lugha ya Kiswahili ili kuweza kuwafikia Watanzania wote kwa urahisi kwa lugha yao mama.

Michuano ya kombe la Dunia ya mwaka huu itaanza kutimua vumbi June 14 hadi Julai 15 huko nchini Russia ambapo jumla ya timu 32 zinashiriki huku bingwa akiondoka na kitita cha dola za kimarekani milioni 38.

Baadhi ya timu zimeshaanza kutangaza vikosi vyao tayari kwa michuano hiyo mikubwa zaidi ya soka hapa Duniani.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment