Responsive image
Responsive image
Posted : May 15, 2018 (a week ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Selemani Jaffo (kushoto) akimhoji mmoja wa wahandisi wa kampuni ya JASCO sababu za kushindwa kutekeleza mradi kwa wakati
Responsive image

Mkandarasi wa kampuni ya JASCO anayetekeleza mradi wa Ujenzi wa barabara zinazojengwa chini ya Mradi wa ULGSP katika manispaa ya Shinyanga amepewa miezi mitatu kukamilisha mradi huo baada ya kusuasua kwa miaka miwili kinyume na mkataba aliosaini.

Akiwa katika ukaguzi wa miradi ya Ujenzi mkoani Shinyanga Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI) Selemani Jaffo  ametembelea mradi huo na kubaini kuwa mkandarasi amejenga kilomita tatu tu kati ya 13.5 mradi ukiwa umeshaongezwa muda mara kadhaa. 

Waziri Jaffo amewaambia viongozi wa kampuni hiyo kwamba baada ya miezi mitatu atatembelea tena mradi huo kuukagua ambapo kama utakuwa haujafika hatua za kuridhisha hatua zaidi zitachukuliwa.

Imeelezwa kuwa mkandarasi huyo amepewa miradi mingi ya ujenzi mkoani humo kiasi kwamba amekosa uwezo wa kuihudumia miradi yote .

VICTORIA PATRICK

MEI 15, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment