Responsive image
Responsive image
Posted : May 14, 2018 (a week ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa Dkt. Hussein Mwinyi
Responsive image

Baadhi ya wabunge wameiomba serikali kuongeza bajeti katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ili kuliwezesha jeshi hilo kuendelea kufanya kazi zake kwa weledi.

Wakichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo iliyowasilishwa Bungeni Mjini Dodoma, wabunge hao wamesema licha ya ongezeko la zaidi ya Shilingi Bilioni mia moja katika Bajeti ya mwaka 2018/2019, bado kuna umuhimu wa bajeti hiyo kuongezwa na kuhakikisha fedha zinazoombwa zinatolewa kulingana na bajeti.

Katika mjadala huo, baadhi ya wabunge wamelipongeza jeshi kwa kuendelea kuhakikisha amani ya nchi inakuwepo huku wakishauri serikali kuhakikisha fedha zinazotewgwa kwa ajili ya jeshi zinatolewa zote.

Aidha baadhi ya wabunge wameunga mkono juhudi za serikali kuendelea kuboresha na hata kuanzisha kambi mpya za Jeshi la Kujenga Taifa ili vijana wote wanaomaliza kidato cha sita washiriki katika mafunzo hayo, hatua ambayo itasaidia kuwajengea vijana uzalendo.

Mapema akiwasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara yake, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la KujengaTaifa Dkt. Hussein Mwinyi pamoja na mambo mengine amesema askari waliouawa mwaka jana nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) walikufa kishujaa na kwamba walipata mafunzo ya kutosha.

Bunge limepitisha makadirio ya zaidi ya Shilingi Trilioni 1.91 yaliyoombwa na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo ili kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha wa 2018/2019.

HOSEA CHEYO

14 MAY 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment