Responsive image
Responsive image
Posted : May 14, 2018 (a week ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
Responsive image

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema tatizo la udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto wa kiume na kike linazidi kuongezeka nchini. .

Akizungumza Jijini Dodoma wakati akifungua Mdahalo wa Wabunge Wajumbe wa Kamati ya Kudumu Huduma za Jamii katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani, waziri huyo amesema matukio ya udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto nchini kwa mujibu wa Jeshi la Polisi yameongezeka kutoka 10,551 mwaka 2016  hadi matukio13,455 mwaka jana. 

Aidha Waziri Ummy amesema vitendo vingi vya ukatili wa kijinsia vimekuwa vinatekelezwa na watu wa karibu na familia. Watoa mada katika mdahalo huu wametaja matatizo mbali mbali yanayosababisha kuvunjika kwa familia. 

Siku ya familia huadhimishwa duniani kote kila tarehe 15 ya Mwezi Mei, ambapo kwa mwaka huu hapa nchini Kauli mbiu ni malezi Jumuishi msingi wa uzalendo utu na maadili ya familia na taifa.

ANETH ANDREW 

14 MEI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment