Responsive image
Responsive image
Posted : May 14, 2018 (a week ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye ulemavu Jenista Mhagama
Responsive image

Serikali imesitisha huduma za utafutaji wa ajira nje ya nchi kwa kampuni tisa ambazo zimebainika kuwa zimekiuka sheria ya huduma za ajira namba 9 ya mwaka 1999.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye ulemavu Jenista Mhagama amesema kampuni hizo zimebainika kuwa na udanganyifu katika huduma ya utafutaji wa ajira nje ya nchi jambo lililopelekea watanzania wengi kuingia kwenye vitendo vya kudhalilishwa huko nje.

.Amesema kuwa serikali pia imebaini watanzania takribani 4,118 wamesafirishwa kwenda nje wengi wao wakiwa hawana ujuzi, kitendo ambacho kimekuwa kikiiweka Tanzania katika sura mbaya katika baadhi ya nchi.

Kwa mara ya kwanza serikali ilisitisha huduma za Mawakala wa Huduma za kazi nje ya nchi Januari 25 mwaka huu na sasa serikali imeweka msimamo kuendelea kusitisha huduma hizo hadi pale Kamishina wa Kazi na Ajira atakaporidhika na matarajio mapya ya kiutendaji kutoka kwa mawakala hao.

HOSEA CHEYO

14 MEI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment