Responsive image
Responsive image
Posted : May 13, 2018 (a week ago) By TBC
Responsive image
Hali ya ulinzi nchini Burundi imeimarishwa baada ya vikundi vya upinzani kutishia kwamba vitahakikisha kura ya maoni haipigwi Mei 17.
Responsive image

Watu wenye silaha wamevamia kijiji kimoja Kaskazini Magharibi mwa Burundi ambapo wamepita nyumba hadi nyumba na kufanya mauaji ya kikatili, ikiwa ni siku chache kabla ya upigaji kura ya maoni kuamua kama Rais Pierre Nkurunzinza aendelee kutawala nchi hiyo hadi mwaka 2034.

Kikundi cha wavamizi kilichotekeleza mauaji hayo ya watu wasiopungiua 26 na majeruhi saba kiliingia katika jimbo la Cibitoke nchini humo kutokea Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, maofisa wamesema.

“Walipita nyumba kwa nyumba huku wakiwa na bunduki na visu na kuchoma moto baadhi ya nyumba” amesema mmoja wa mashuhuda.

Wachambuzi wamesema shambulio hilo linaweza kuwa ni jaribio la kutaka kusimamisha kura ya maoni inayotarajiwa kupigwa wiki ijayo kuamua kama Rais Nkurunzinza aendelee kutawala.

Rais Nkurunziza ametawala Burundi tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza mwaka 1994 vilipomalizika nchini humo mwaka 2005, lakini azma yake ya kujiongezea muhula wa tatu mwaka 2015 iliingiza nchi hiyo katika machafuko mapya.

Kura ya ndio katika upigaji kura ya maoni inayotarajiwa wiki ijayo, itamwezesha Rais huyo kuendelea kugombea  urais kwa vipindi viwili zaidi vya miaka saba kila kimoja.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment