Responsive image
Responsive image
Posted : May 12, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Kilimo Charles Tizeba
Responsive image

Waziri wa Kilimo Charles Tizeba ametoa onyo kwa mfanyabiashara yeyote atakayepandisha bei ya sukari kwa kisingizio cha uhaba wa sukari nchini.

Waziri Tizeba ametoa onyo hilo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema kuwa Sukari ipo ya kutosha nchini na inakidhi mahitaji ya wananchi.

Onyo la Waziri Tizeba limekuja baada ya kuwepo  kwa taarifa kuwa baadhi ya wanyabiashara wamekusudia kupandisha bei ya sukari. 

Waziri TZEBA amesema baada ya manung’uniko ya kuwepo tishio la kupanda kwa bei ya sukari imemlazimu kufanya mazungumzo na wafanayabiashara wakubwa wa sukari na amejiridhisha kuwa hakuna uhaba wa bidhaa hiyo nchini.

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment