Responsive image
Responsive image
Posted : May 12, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina
Responsive image

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina amezindua operesheni  Nzagamba yenye lengo la kukomesha usafirishaji wa mifugo nje ya nchi bila vibali unaosababisha upotevu wa mapato katika sekta mifugo na mazao yake, pamoja na kudhibiti uingizaji wa dawa bandia za mifugo nchini.

Waziri Mpina amezindua operesheni hiyo wilayani Longido Mkoa wa Arusha ambapo pia amefanya ukaguzi katika kiwanda cha kufungasha dawa za mifugo cha Ultravetis kilichopo Jijini Arusha.

Baada ya ukaguzi huo waziri huyp akawataka wamiliki wa kampuni hiyo kuacha kujihusisha na tabia ya kuuza dawa bandia jambo linalosababisha mifugo mingi kufa na kuwapa hasara wafugaji.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Longido, Daniel Chongolo amesema tayari wameshapata mwekezaji anayejenga kiwanda cha kusindika nyama kitakachosaidia kupunguza usafirishaji wa mifugo

SECHELELA KONGOLA

12 MAY 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment