Responsive image
Responsive image
Posted : May 11, 2018 (2 weeks ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo
Responsive image

Serikali imeziagiza halmashauri zote nchini kutoa fedha za mikopo ya asilimia kumi ya mapato yao kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu bila kuwatoza riba yoyote.

Agizo hilo limetolewa jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Magomeni.

Jaffo ameagiza halmashauri zote nchini  zitoe mikopo kutokana na asilimia kumi ya mapato yao ili kuwafikia wanawake kwa asilimia nne, vijana asilimia nne na watu wenye mahitaji  maalum asilimia mbili.

Waziri huyo pia akawahakikishia wafanyabiashara wa eneo hili linapojengwa soko la kisasa, kupata nafasi ya kufanya biashara zao pindi ujenzi utakapokamilika.

Kwa upande wake afisa masoko wa wilaya ya Kinondoni, Zahoro Hanuna amesema ujenzi wa soko hilo la kisasa unatarajia kukamilika Disemba  mwaka huu.

Takribani shilingi bilioni tisa zinatarajia kutumika katika ujenzi wa soko la Magomeni ikiwa ni utekelezaji wa azma ya serikali ya kuboresha masoko na vituo vya mabasi nchini. 

AGNES MBAPU

11MAY 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment