Responsive image
Responsive image
Posted : May 03, 2018 (3 weeks ago) By TBC
Responsive image
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Marco Mtunga
Responsive image

Serikali imewafutia wakulima wa zao la pamba nchini deni la Shilingi Bilioni 30 lililotokana na chupa Milioni saba za viatilifu walizopatiwa kwa njia ya mkopo katika msimu wa kilimo wa mwaka 2017/2018.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Marco Mtunga amesema  uamuzi wa kufuta deni hilo umelenga kuwaondolea wakulima mzigo wa madeni ambapo sasa watalazimika kulipia mbegu pekee.

Kufutwa kwa deni hilo ambalo wakulima walitakiwa kulilipa baada ya kuuza Pamba ni ahueni kwa wakulima kutokana na bei ya Pamba mbegu kupungua kutoka shilingi 1200 kwa kilo moja mwaka 2017/2018 hadi shilingi 1100 mwaka 2018/2019.

Ili kuhakikisha wakulima wanazalisha Pamba kwa Tija, Mtunga amesema serikali itaimarisha huduma za ugani na kuwapatia wakulima pembejeo ikiwemo viatilifu na mbegu bora aina ya UK M 08 kuanzia msimu ujao wa kilimo bila malipo.

Mei mosi mwaka huu, Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba amezindua msimu wa ununuzi wa pamba kitaifa katika wilaya ya Igunga Mkoani Tabora na kusema dhamra ya serikali ni kuwezesha wakulima wa Pamba kunufaika na kilimo.

Zaidi ya Kilogram Milioni 600 zinatarajiwa kuvunwa nchini msimu huu kutoka eneo lililopandwa la zaidi ya ekari millioni tatu.

REGNALD NDESIKA

03 MAY 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment