Responsive image
Responsive image
Posted : May 02, 2018 (3 weeks ago) By TBC
Responsive image
Eneo ambapo mshambuliaji wa kujitoa mhanga amejilipua mjini Tripoli, Libya
Responsive image

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga walau mmoja amejilipua nje ya jengo la makao makuu ya Tume ya Uchaguzi mjini Tripoli Libya na kusababisha vifo vya watu 12 na majeruhi kadhaa.

Wakati tukio hilo likitokea washambuliaji wengine walivamia ndani ya jengo hilo la Tume na kuwasha moto.

Msemaji wa Tume ya Uchaguzi Khaled Omar ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba maofisa watatu wa tume hiyo pamoja na maofisa usalama wanne ni miongoni mwa watu waliouawa katika shambulio hilo.

Omar amesema aliwaona washambuliaji wakivamia jengo hilo na baada ya mmoja wao au wawili kujilipua aliona vipande vya miili yao imekatika vipande vipande ardhini.

Hakuna kikundi chochote ambacho kimedai kuhusika na shambulio hilo lakini watu wengi wanaamini wapiganaji wenye uhusiano na kikundi cha Islamic State ndio waliohusika.

Libya imekuwa katika machafuko tangu Rais wao Muammar Gaddafi alipoondolewa madarakani mwaka 2011 baada ya utawala wake wa miaka 42.

Wananchi wa Libya wamekuwa wakijiandikisha kupiga kura katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika baadae mwaka huu na shambulio hilo katika makao makuu ya Tume ya uchaguzi linapeleka ujumbe kwamba uchaguzi huo unapingwa na baadhi ya watu au vikundi.

Ingawa wachambuzi wengi wana wasiwasi kama uchaguzi huo utakuwa salama katika nchi iliyogawanyika kisiasa na kijeshi, jumuia ya kimataifa inaonekana kuwa na matumaini kwamba uchaguzi huo utaipa nchi hiyo mwanzo mpya.

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment