Responsive image
Responsive image
Posted : April 25, 2018 (4 weeks ago) By TBC
Responsive image
Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
Responsive image

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema maambukizi ya ugonjwa wa malaria nchini yameshuka kutoka asilimia 14 ya mwaka 2015 hadi  asilimia 7.3 mwaka 2017.

Waziri Ummy ametoa takwimu hizo katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ambayo kitaifa yamefanyika wilayani Kasulu Mkoani Kigoma, wilaya ambayo ina kiwango cha juu cha maambukizi ya ugonjwa huo ikilinganishwa na maeneo mengine nchini.

Kupungua kwa  kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa malaria nchini kunatajwa ni kutokana na jitihanda mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tano katika sekta ya afya ikiwemo kuongeza vifaa tiba, dawa pamoja na watoa huduma.

Kwa upande wake Waziri Elimu, Sayansi na Teknolijia Prof, Joyce Ndalichako ambae nae amehudhuria maadhimisho hayo ameunga mkono jitihada za kuutokomeza ugonjwa wa malaria huku akiahidi kuanzisha somo la afya katika shule za msingi na sekondari nchini.

ABDULATIF SAID

25 APRILI 2018

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment