Responsive image
Responsive image
Posted : April 20, 2018 (a month ago) By TBC
Responsive image
Rais Dkt John Magufuli
Responsive image

Rais Dkt John Magufuli ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa zinazoenea mitandaoni juu ya upotevu wa shilingi trilioni 1.5 zinazodaiwa kutoka kwenye ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa serikali (CAG) na kusema kuwa taarifa hizo si za kweli ambapo amewataka watanzania kutoamini kila kinachoandikwa kwenye mitandao ya kijamii.

Rais Magufuli ameyasema hayo mara baada ya kuwaapisha majaji kumi wa mahakama kuu, Naibu mwanasheria mkuu wa serikali, Naibu mkurugenzi wa mashtaka, Wakili na Naibu wakili mkuu wa serikali ambapo amewataka wakatekeleze majukumu yao kwa kufuata haki.

Katika hafla hiyo, Waziri wa katiba na sheria Profesa Malamagamba Kabudi na Kamishna wa maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela wamewataka watumishi hao wa mahakama kufuata maadili.

Naye Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma amesema majaji hao wana jukumu la  kupunguza mashauri yaliyopo mahakamani.

Wakati huo huo Rais Dkt. John Magufuli amemteua Msalika Makungu kuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Tabora. Taarifa iliyotolewa na Ikulu imesema Makungu anachukua nafasi ya Dkt. Thea Ntara ambaye amestaafu.Uteuzi wa Makungu umeanza leo na tarehe ya kuapishwa kwake itapangwa baadaye.

KHALID GANGANA

APRILI 20, 2018

 

Responsive image
HABARI ZINAZOHUSIANA
MAONI YA WASOMAJI

Leave Your Comment